Chuo Kikuu cha Theolojia cha Mtandaoni.
Swali #2:
Kwa kutumia uelewa wa kimuktadha na kihistoria wa
Mdo 4:29, 31 SUV
“Basi sasa, Bwana, yaangalie matisho yao; ukawajalie watumwa wako kunena neno lako kwa ujasiri wote, Hata walipokwisha kumwomba Mungu, mahali pale walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri.”
Thibitisha usemi huu: mkakati (mbinu) mkubwa wa kanisa ni maombi. Kwa kadiri kanisa linavyokosa mbinu mbadala na nyinginezo ndivyo hushinda kwa namna ya kimiujiza; na kwa jinsi ambavyo kanisa huwa na mbinu nyinginezo na mbadala wa maombi ndivyo ambavyo hudhoofu na kuhitaji uamsho ambao huja kwa kufunikwa na roho ya maombi. (Alama 30)