Chuo Kikuu cha Theolojia Mtandaoni 😊

Baada ya muda nikajiridhisha kwa namna ya kibinadamu inawezekana hizo ndoto na maono zilikuwa ni “ndoto tu”; huenda yalikuwa ni mawazo ya utotoni; huenda nilikuwa bwana ndoto (Unakumbuka Yusufu mwana wa Yakobo alivyotungiwa jina).

Hatimaye nikaanza kuelekea uelekeo wangu ninaouelewa mwenyewe. Nitajenga ndoto ya kuwa mwanataaluma nguli – Profesa na Mtafiti… nilipenda kuwa Prof. JK

Kumbe akitiye mbinguni anacheeeeeeeeeeeka 🤣

Anyways, tuyaache hayo…

Mara “Nasikia kuitwa!” 🫣

Kama ningekuwa Profesa sasa nikapata nafasi ya kutunga maswali… Basi, yangesomeka hivi:

“… ni vigumu kwako kuupiga mateke mchokoo…” Matendo ya Mitume 26:14
Kwa kuzingatia muktadha wa andiko fafanua ni kwa jinsi kulizuia kanisa ni kufupiza muhula wako (Alama 30)